12 août 2022

KAULI YA MHESHIMIWA WAZIRI WA HAKI ZA BINADAMU, USTAWI WA JAMII NA JINSIA KUHUSU MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA WATU WENYE ULEMAVU, TOREO YA 2018

Ndugu zanguni, Mabibibi na mabwana;

1.     Desemba 3 ya kila mwaka, ulimwengu wote unadhimisha siku ya kimataifa ya watu wenye ulemavu.

2.

Martin NIVYABANDI, Mheshimiwa Waziri wa Haki za Binadamu, Ustawi wa Jamii na Jinsia (file Photo par Elie HARINDAVYI)

Ili Serikali ya Jamhuri ya Burundi iweze kukuza na kulinda haki za watu wenye ulemavu, hatua kadhaa zilifanika kupitia Wizara inayohusika na Haki za Binadamu, Jamii na Jinsia, lakini pia kupitia na Wizara zingine zinazohusika. Hizi ni pamoja na elimu na ukarabati wa kimwili, mafunzo katika taaluma mbalimbali na utoaji wa vifaa vya uhamaji, mafunzo katika kiufundi mbalimbali na kutoa kitengo cha kuingilia tena, msaada katika shughuli za kuzalisha mapato kwa vituo na vyama kwa watu wenye ulemavu, kuwepo kwa shule za majaribio katika mfumo wa elimu ya pamoja, huduma ya bure kwa wanawake wanajifungua na watoto wenye umri chini ya miaka mitano (05), bila kuacha kando aina mbalimbali za chanjo zinazotolewa kwa watoto na wakina mama ambao kwa njia moja au nyingine huchangia kuzuia ulemavu, nk.

3.     Sera ya Ulinzi wa Jamii na Mkakati wake wa utekelezaji vilianzishwa, kama vile Mfuko wa Usaidizi wa Jamii (FAPS).  Tarehe 26 mwezi Machi 2014, Serikali ya Burundi iliidhinisha Mkataba wa Kimataifa juu ya Haki za Watu wenye ulemavu. Na  ni furaha kuu ya kutoa kauli hii wakati Sheria juu ya Kukuza na Kulinda Haki za Watu wenye Ulemavu ilitangazwa rasmi Januari 10 mwaka huu.

4.     Hata ingawa mengi yamefanyika kwa watu wenye ulemavu, bado kuna njia ndefu ya kwenda, kutokana na mahitaji makubwa ya jamii hii ya watu walio na mazingira magumu. Kwa hiyo, pamoja na siku ya ushirikiano wa ndani ambayo ilizinduliwa mwaka jana na sheria hii inayolenga na kulinda haki za watu wenye ulemavu, Sera ya Ulemavu ya Kitaifa na Mpango wake wa Utekelezaji vimeandaliwa.

5.     Tungependa kutoa shukrani za dhati kwa watu wote na mashirika mbalimbali ambao hujitoa kwa hali na mali, kwa moyo na nafsi zao wakifanya kazi kwa watu wenye ulemavu.

6.     Maadimisho ya Sherehe hiyo itakuwa Jumatatu, tarehe 3 Desemba mwaka wa 2018, na siku hii itadhihirishwa na ziara katikati kituo cha watu viziwi wa « EPHPHATA » pamoja na uthibitisho wa Sera ya Kitaifa ya Watu Wenye Ulemavu na Mpango wake wa utekelezaji.

7.     Kwa watu wote wenye ulemavu, tunawaambia, sikukuu njema!                               

Mungu awabariki, asanteni sana !!

Elie HARINDAVYI

Le Coordonnateur de la Cellule de Communication et d'Information du Ministère des Droits de la Personne Humaines, des Affaires Sociales et du Genre

Voir tous les articles de Elie HARINDAVYI →