KAULI YA MHESHIMIWA WAZIRI WA HAKI ZA BINADAMU, USTAWI WA JAMII NA JINSIA KUHUSU UWANZIRISHAJI WA KAMPENI YA SIKU 16 ZA KUTOKOMEZA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WASICHANA, TOLEO LA 2019

Na Elie HARINDAVYI

1.       Mnamo Novemba 25 ya kila mwaka, Burundi inajiunga na nchi zingine za ulimwengu katika kuzindua rasmi Kampeni ya Siku 16 ya uharakati dhidi ya ukatili kwa wanawake na wasichana. Kipindi hiki kinaanza Novemba 25 na kuisha Disemba 10.

Mheshimiwa Waziri wa Haki za Binadamu, Ustawi wa Jamii na Jinsia akisoma Tangazo jana juma pili tarehe 24 novemba 2019 katika jiji la Bujumbura (Picha na Elie HARINDAVYI)

2.       Kampeni hii ni fursa ya kukumbuka wanawake na wasichana waathirika kutokana na unyanyasaji mbali mbali. Ni wakati wa kujitathmini kwa wadau wa sekta ya kupambana na unyanyasaji wa kijinsia ili waweze kuendeleza mafanikio na kupitisha mikakati bora ya kushinda unyanyasaji wa kijinsia, vizuizi na changamoto zinazoendelea.

3.       Mada ya kitaifa  mwaka huu ni Acha  Burundi iangaze: sisi sote tumalize ukatili dhidi ya wanawake na wasichana. « 

4.       Maada hii ilichaguliwa ili kupeana dhamiri ya kila mtu kuhusika zaidi katika vita dhidi ya jambo hili ambalo linadhoofisha ubinadamu wote, na linaitaji kazi ya ushirikiano wa washirika tofauti kujenga Burundi ambayo inang’aa.

5.       Siku hii inafika wakati Serikali ya Burundi inaendelea kuimarisha hatua zake katika mapambano dhidi ya ukatili kwa wanawake na wasichana kupitia shughuli za kukuza uwezeshaji binafsi na kinga bora dhidi ya janga hilo.

6.       Wakati wa Kampeni hii, shughuli kadhaa zitaandaliwa nchini kote wakizungumzia maada hiyo; haswa, usambazaji wa sheria maalum ya Kuzuia, ya ulinzi wa wahasiriwa na kutokomeza Ukatili wa Kijinsia kwa viongozi tofauti katika ngazi zote.

7.       Katika ngazi ya kitaifa, uzinduzi rasmi wa Kampeni ya Siku 16 ya uharakati dhidi ya Ukatili dhidi ya Wanawake, toleo la 2019, itafanyika Jumatatu Novemba 25, 2019 tarafani BUGENYUZI katika mkoa wa KARUSI.

8.       Kwa niaba ya selikari tunatoa wito kwa Burundi wote, haswa wenyeji wa tarafa ya Bugenyuzi, kuja kwa wingi katika sherehe za kuzindua rasmi  Kampeni hii na kushiriki katika shughuli ambazo zitaandaliwa wakati wa kipindi hiki.

9.       Kwa warundi wote, tunawatakia maisha mema, bila ukatili  dhidi ya wanawake na wasichana!10.  Asanteni sana! Mungu awabariki!

Comments are closed.