29 mars 2024

KAULI YA WAZIRI WA HAKI ZA BINADAMU, USTAWI WA JAMII NA JINSIA KUHUSU MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO MWAFRIKA, TOLEO LA MWAKA 2019

  1. Maadhimisho ya siku ya mtoto mwafrika tarehe 16 Juni ya kila mwaka aliamuliwa na Umoja wa Afrika chini ya azimio CM/RES1290. Ni fursa ya kukumbuka mauaji ya watoto wa Soweto mwaka 1976, kufuatia mandamano ya kudai haki yao ya elimu isiyozingatia kanuni ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika ya Kusini; Ilikuwa nyenzi ya utawala wa kibaguzi apartheid.
  2. Martin NIVYABANDI, Waziri wa Haki za Binadamu, Ustawi wa Jamii na Jinsia alipokua anasoma tangazo hilo

    Mada iliyopendekezwa na kamati ya Afrika ya wataalamu kuhusu mkataba wa Afrika kuhusu haki na ustawi wa mtoto na iliyopitishwa na Baraza la utendaji la kwa mwaka 2019, ni ifuatawo: « shuguri za kibinadamu barani Afrika: haki za mtoto juu ya yote« . katika nchi yetu, serikali imeona ni bora kuwa na mada hii .inazipa kipaumbele haki za mtoto mahali popote na katika hali zote ikiwa pamoja na katika mazingira ya kibinadamu.

  3. Maadhimisho ya siku hii huja wakati Burundi inajitahidi kuhakikisha kwamba  haki za mtoto zinalindwa kikamilifu. Ni muhimu kutaja miongoni mwa mambo mengine utekelezaji wa mkakati wa serikali wa kutoa watoto wanaoishi barabarani na kuarudisha katika familia zao . Tangu utekelezaji wa mkakati huu hadi sasa, zaidi ya watoto 3500  wamekuwa  wameunganishwa na familia zao.
  4. Mfano wa pili ni kampeni inayoendelea taifa nzima kwa lengo ya kupambana na uzembe juu ya maisha ya watoto .Utelekezwaji umezinduliwa rasmi  mwaka 2017 Novemba. Kampeni hii itakuwa na sifa ya kushughurikia  changamoto ya kupambana na kutelekezwa katika wanja wa usafi, elimu, chakula, afya na mambo mengine mengi. Uhamasishaji kwa dhamira juu ya  haki za watoto umekuwa unafanywa. Hapa Tunakaribisha uwajibikaji uliofanywa na wasimamizi wote wa kijamii kuinua kiwango ca msaada kwa watu walio katika hatari wakati wa upangaji wa bajeti.
  5. Kwa upande wa mkakati na dhamira hii, serikali aliweka siku wakfu kwa mshikamano katika jamii (Jumamosi ya mwisho wa mwezi Julayi), ambayo itachangia katika kuboresha kabisa hali ya mtoto kwa ujumla na watoto walio hatarini . Aidha, sera ya Taifa ya ulinzi wa mtoto imeundwa na hivi karibuni utapelekwa kwa tasisi husika  kwa ajili ya kupitishwa. Na sawasawa kuhusu sheria inayolenga  ulinzi wa mtoto.
  6. Serikali ya Burundi inathibitisha utashi na ahadi wake kuhakikisha ulinzi kamili wa watoto wote na kusaidia familia.
  7. Katika nchi yetu, maadhimisho atafanyika tarehe 18 Juni 2019 kata  ya Buterere ,jijini Bujumbura.
  8. Tukuchukua fursa hii kuwaalika wenyeji wa Buterere na maeneo yanayozunguka eneo hilo kuja  wengi  kuhudhuria sherehe hizi.
  9. Tunatakieni siku kuu njema watoto wote wa Burundi na bara la Afrika

ASANTE

Elie HARINDAVYI

Le Coordonnateur de la Cellule de Communication et d'Information du Ministère des Droits de la Personne Humaines, des Affaires Sociales et du Genre

Voir tous les articles de Elie HARINDAVYI →