29 novembre 2023

KAULI YA MHESHIMIWA WAZIRI WA HAKI ZA BINADAMU, USTAWI WA JAMII NA JINSIA KUHUSU MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA WAZEE, TOREO YA 2018

1. Tarehe mosi Oktoba kila mwaka, dunia inaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wazee.

 2.  Mwaka huu mandha ya kimataifa na pia iliyochaguliwa katika nchi yetu ni « Kuadhimisha mabingwa wa haki za wazee. »

 3. Katika mazingira ya kuhifadhi jamii, hatua zifuatazo zimechukuliwa na Serikali ya Burundi:

 kutiwa saini makubaliano ya kushirikiana na Vituo na Mashirika anaofanya kazi kwa manufaa ya wazee kama  kupewa  msaada wa kifedha kila mwaka, kulipa   bili za maji na umeme na msamaha wa ushuru kwa bidhaa na huduma kutoka nje kwa ajili ya kuasadia wazee; kutembelea na kugawa  msaada wa chakula na vifaa mhimu   kwa vituo na mashirika hayo, msaada wa matibabu kwa wazee walio katika hali duni; Pensheni na kadi ya Shirika la ku hudhumia kiafya wafanya kazi wa selikari   hutolewa kwa wastaafu.

 4. Pia, katika mwaka  wa 2012, Serikali yetu imepitishwa Sera ya Taifa kwa ajili ya Ulinzi wa Jamii na Mkakati wa utekelezaji wake ni tayari katika mahali pamoja na Mfuko wa Msaada kwa ajili ya Hifadhi ya Jamii « FAPS ». Mkakati huu na mfuko vinatilia manani makundi ya wasiyojiweza kwa ujumla na hasa wazee.

 5. Ijulikane kwamba , nchi yetu ina mpango wa maendeleo wa Taifa (2018-2027) ilizinduliwa tarehe 22 Agosti mwaka huu na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya katika mkoa wa Gitega na mapendekezo  maalumu ametolewa kwa taasisi zinawapa hudhuma mbalimbali watu wazee .

6. Mbali na utafiti wa upembuzi  kwa ajili ya kutoa hudhuma bure  ya afya kwa faida ya wazee wote  imegharimiwa na Serikali ya Burundi,  pia ilipendekeza kwamba taasisi zinazoshughurika  na mambo ya ustaafu  kutafuta njia ya  kuboresha kiwango ca kiinua mgongo . Zaidi ya hayo, Shirika  la Brothers ‘BENEYOZEFU « limefanya utafiti juu ya  mahitaji ya wazee katika baadhi ya matarafa na tunatarajia kuona matokeo ya hiyi kazi.

 7. Licha ya  hatua hizi zote zilizopigwa na Serikali, ingali kazi kubwa  sababu kuna watu wazee ambao bado wako katika hali mbaya sana na wengine kuwa tu wameondolewa hivi karibuni mitaani. Kwa matatizo yote wazee wanakabiliwa nayo , Serikali ya Burundi ina utashi wa kufanya kila juhudi  kulingana na uwezo wake ili ihudhumie wazee. Tuna uhakika kwanba hakuna njia yingine ya kufaulu bila kupitia mfumo wa mshikamano vijijini,mfumo  ambayo umezinduliwa Julai mwaka huu.

 8. Katika nchi yetu, siku ya kimataifa ya wazee itaadhimishwa tarehe mosi Jumatatu, Oktoba  2018 katika Mkoa wa  Gitega, tarafani Giheta ambako itajadiliwa swala kuhusu  msaada kwa wazee katika mazingira magumu na pia  kufuata matokeo  ya utafiti juu ya  mahitaji ya wazee uliofanywa na Shirika la Brothers ‘BENEYOZEFU « kwa msaada wa World Solidarity Organization .

 9. Tatimaye ,tunachukua hiyi fursa  kutoa shukrani za dhati kwa vituo, mashirika na mtu yeyote kwa changia katika kuhifadhi wazee na kukaribisha kila mtu kufanya hivyo na kua mfadhili.

 10. Siku kuu njema  kwa wazee wote!

 IDUMU  BURUNDI;

TUSHIRIKIANE KWA KUWAHUDHUMIA WAZEE;

MWENYEZI MUNGU AWABARIKI, ASANTENI !!

 

Elie HARINDAVYI

Le Coordonnateur de la Cellule de Communication et d'Information du Ministère des Droits de la Personne Humaines, des Affaires Sociales et du Genre

Voir tous les articles de Elie HARINDAVYI →